Video Bar

Loading...

Sunday, 25 February 2018

Donating blood is a safe and easy process which gives you the chance to change lives.


Donating blood is a safe and easy process which gives you the chance to change lives.
It is not possible to get AIDS or other infectious disease by giving blood.
A brand new, sterile, disposable needle is used for each blood donation. Once used, the needle is discarded.
You can only donate if your health history permits and you feel well. You are asked general health questions and are given a mini physical – temperature, pulse, blood pressure and hemoglobin are checked – prior to donation to ensure that you are feeling well and that it is safe for you to give blood. Your health history and test results are confidential and cannot be shared without your permission.
Kuchangia damu ni salama na rahisi na pia unapata fursa ya kubadili maisha ya wengine.
Hauwezi kupata UKIMWI au magonjwa mengine ya kuambukiza kwa kuchangia damu.
sindano mpya hutumika kwa kila mchangia damu.
Unaweza tu kuchangia kama historia yako ya afya inaruhusu na unajisikia vizuri. utaaulizwa maswali ya afya ya jumla na utapimwa shinikizo la damu, wingi wa damu,kabla ya kuchangia ili kuhakikisha kuwa unajiskia vizuri na ni salama kwako kutoa damu. Historia yako ya afya na majibu ni ya siri na haiwezi kutolewa bila idhini yako.
Tuesday, 13 February 2018

MAKUNDI YA WATU WANAOHITAJI KUONGEZEWA DAMUMakundi katika jamii yanayohitaji damu mara kwa mara ni:-

wadogo hasa walio chini ya umri wa miaka mitano.
Majeruhi wa ajali mbalimbali hasa ajali za barabarani.
Wajawazito na wanawake wenye matatizo ya uzazi.
Watu wanaofanyiwa tiba ya upasuaji.
Wale wote wenye magonjwa mbalimbali yanayosababisha upungufu wa damu

TAFADHALI ZINGATIA HAYA BAADA YA KUCHANGIA DAMUWednesday, 7 February 2018

SERIKALI YAHIMIZA TAASISI NA VIKUNDI MBALIMBALI KUSAIDIA HAMASISHA JAMII KUCHANGIA DAMU KWA HIARI
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu(MB) amehimiza Taasisi na Vikundi mbalimbali vya Sanaa kuiga mfano wa Chama cha Wanawake wa Tasnia ya Filamu Nchini katika kuelimisha na kuhamasisha jamii kuhusu umuhimu wa kuchangia damu kwa hiari. Hayo yamesemwa leo na Waziri wa afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na watoto, Ummy Mwalimu wakati wa uzinduzi wa kampeni ya kuchangia katika viwanja vya Biafra, Kinondoni Dar-es-salaam, Kampeni ambayo inaratibiwa na Chama cha Wanawake wa Tasnia ya filamu kwa kushirikiana na Mpango wa taifa wa Damu Salama, Kanda ya Mashariki.
Waziri Ummy amesema Serikali inatambua mchango wa Taasisi na Vikundi mbalimbali hapa Nchini katika kusaidia kuhamasisha Wananchi kuchangia damu kwa hiari mara kwa mara kwani maisha ya watu wengi yanaokolewa kwa kuongeza damu, Waziri Ummy alisema kina mama wengi na watoto hupoteza maisha kwa kukosa Damu na takwimu za hivi karubuni zinaonyesha kina mama 556 katika kila vizazi hai 100,000 hufariki kila mwaka na inakadiriwa asilimia 40 ya vifo hivyo husababishwa na ukosefu wa Damu.
Mbali na hayo Waziri Ummy amesema jukumu la kuhakikisha upatikanaji wa Damu ya kutosha na iliyosalama ni la wadau wote wakiwemo viongozi wa Idara za serikali, wanasiasa, na taasisi zisizo za kiserikali. Hivyo ni vyema wadau wote watambue kuwa ni wadau muhimu wa Mpango wa Taifa wa Damu salama na hawana budi kutoa ushirikiano pale wataalamu wa Mpango wa Taifa wa damu salama wanapofika katika maeneo yao.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama cha wanawake wa Tasnia ya Filamu nchini Vanita Omary amesema lengo la kampeni hiyo ni kufikisha chupa 300 za damu katika uzinduzi huo na tayari washapata chupa 288 mpaka sasa tangu walipoanza endesha kampeni kwa kushirikiana na Damu salama kanda ya mashariki.


Saturday, 14 March 2015

MFUKO WA TAIFA WA BIMA YA AFYA TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

 

                                                      


 

ZOEZI LA UPIMAJI WA AFYA NA KUKUSANYA DAMUSALAMA KWA USHIRIKIANO WA NHIF NA MPANGO WA TAIFA WA DAMU SALAMA KATIKA MIKOA SITA (6) MACHI 2015

Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) kwa kushirikiana na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kupitia Mpango wa Taifa wa Damu Salama, utaendesha zoezi la upimaji wa afya nakukusanya damu salama katika maeneo mbalimbali nchini ili kupunguza tatizo la uhaba wa damu salama kwa matumizi ya wagonjwa nchini na wakati huo huo kuwawezesha wananchi kujua afya zao na hivyo kuchukua hatua stahiki mapema.

Hatua hii imefikiwa baada ya kuwepo kwa tatizo la uhaba wa damu salama katika vituo vya matibabu nchini, ambavyo vingi vinahudumia wanachama wetu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya.

Tumetaarifiwa na wenzetu wa Damu salama kuwa mahitaji yadamu salama nchini ni chupa 400,000 hadi 450,000 za ujazo wa mililita 450 kwa mwaka ambayo ni sawa na wastani wa chupa 106 za damu kwa robo moja ya mwaka. Hata hivyo, kutokana na kutofikia kiwango hicho, Mpango wa Damu Salama Tanzania ilijiwekea lengo la kukusanya chupa 150,000 kwa kipindi cha mwaka jana ambayo ni sawa na lengo la kukusanya chupa 37,500 kwa robo mwaka. Hili ni suala la dharura na linahitaji hatua za haraka na ushirikiano miongoni mwa wadau wa sekta ya afya na wananchi kwa ujumla.

Takwimu zilizopo zinaonyesha kuwa kiasi cha chupa 19,000 za damu salama zilikusanywa katika kipindi cha robo mwaka cha Octoba – Desemba 2014, wakati ambapo chupa 18,000 zimekusanya kwa kipindi cha kuanzia Januari 2015 hadi sasa. Hii inaonesha wazi kuwa upo uhaba mkubwa wa damu kulinganisha na uhitaji uliopo hasa katika vituo vikubwa mfano Muhimbili ambapo zinahitajika chupa 50 hadi 60 za damu kwa siku.

Kutokana na umuhimu na uharaka wa suala hili na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya 

(NHIF) umeona ni vema kuunga mkono juhudi za Serikali katika kipindi hiki cha uhaba mkubwa wa damu salama kwa kushirikiana na Taasisi ya Mpango wa Damu Salama na wadau wengineo kwa kufanya zoezi la ukusanyaji wa damu kutoka kwa uchangiaji wa hiari wa wananchi. 

Zoezi hili litaambatana na zoezi la uhamasishaji wa wananchi kuhusu umuhimu wa kujiunga na Bima ya afya pamoja naupimaji wa afya kwa magonjwa yasiyoambukiza (kama sukari, shinikizo la damu na hali lishe) ambalo hufanywa na Ofisi za Mikoa za NHIF kila robo ya mwaka. 

Zoezi hili litafanyika katika mikoa ya Dar es Salaam, Mwanza, Tabora, Kilimanjaro, Mtwara na Mbeya na linategemewa kuanza tarehe 23 Machi, 2015 katika vituo vifuatavyo:-

SN

MKOA HUSIKA

KITUO CHA UKUSANYAJI

1

Dar es Salaam

Gongo la Mboto Stand

Karume Sokoni, 

Mlimani City, 

Mbagala Stand, 

Banana Stand, 

Buguruni Stand.

2

Mwanza

Igoma Stand, 

Pasiansi Stand, 

Buswelu Center, 

Buhongwa Center na 

Nyegezi Stand.

3

Mbeya

Viwanja vya Shule ya Msingi Mwegeishi na Gombe, 

Viwanja vya Mbata na Rundazove, 

Mbalizi Stand na 

Uyole.

 

4

Kilimanjaro (Moshi)

Mwika stand

Soko la Chekereni (Kahe)

Kwa Sadala (Hai), 

Soko la Siha, 

Soko la Lawate (Siha), 

Soko la Kwa Mangula (Rombo)

 

5

Tabora

Viwanja vya Ndala TTC, 

Urambo Center, 

Kaliua Center, 

Usoke Center na 

Town Center  

6

Mtwara

Hiyari Center, 

Nanyamba Center, 

Naliendele Center, 

Umoja Center na Mikindani Center.

 

 

NHIF pamoja na Mpango wa Damu salamu tunaungana na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kutoa wito kwa wananchi kuona hitaji lililopo na kushiriki kikamilifu katika zoezi hilitukijua kuwa ugonjwa huja bila taarifa, na ugonjwa waweza kumtokea yeyote na akahitaji kuongezwa damu. Majeruhi wengi wa ajali huhitaji msaada wa damu, hivyo tunawahimiza na kuwahamasisha Wananchi  kutoa kipaumbele katika suala hili na kujitokeza kwa wingi kuchangia kwa hiari damu katika vituo vilivyoainishwa.

 

Ni matarajio yetu kuwa kama kila kitu kitakwenda sawa, tunatarajia wananchi 6,000 watajitokeza kuchangia damu na sisi wenyewe katika Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya tutakuwa miongoni mwa washiriki wa kwanza kuchangia. 

Ni matarajio yetu pia kuwa wananchi wengi zaidi watajitokeza kupima afya na kupata elimu ya bima ya afya ambayo tumekuwa tukiitoa kata kwa kata. Safari zoezi la kata kwa kata litafanyika katika maeneo tuliyotaja, hivyo tunawahimiza wajitokeze kwa wingi kupima afya.

Aidha napenda nimalizie kwa kuwashukuru wana habari na kuvipongeza sana vyombo vya habari kwa kushiriki katika kuhamasisha jamii na katika kampeni hii ambayo kwa kweli inaokoa maisha ya watanzania wengi wakiwemo wanachama wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya.

Nawashukuru sana.

 

Imetolewa na:

Kaimu Mkurugenzi MkuuMfuko wa Taifa wa Bima ya Afya,

Kwa kushirikiana na

Mpango wa Damu Salama Tanzania,

14/03/2015

1

 

Donating blood is a safe and easy process which gives you the chance to change lives.

Donating blood is a safe and easy process which gives you the chance to change lives. It is not possible to get AIDS or other infectiou...